Meli ya Handala Yakabiliwa na Hatari ya Kukamatwa na Jeshi la Israeli
Meli ya misaada ya kibinadamu iitwayo Handala, iliyotumwa na muungano wa wanaharakati wa kimataifa wa Freedom Flotilla Coalition, inakaribia ukanda wa Gaza huku ikikabiliwa na tishio la kukamatwa na Jeshi la Majini la Israeli. Meli hiyo iliondoka kutoka Syracuse, Italia mnamo Julai 13, ikiwa na wanaharakati 19 na waandishi wa habari 2, kwa lengo la kuvunja mzingiro wa baharini wa Gaza unaodaiwa kuwa wa kinyume cha sheria
Kauli ya Israeli
Tutakamata meli ya Handala ikiwa haitakubali kurudi nyuma
Jeshi la Israeli limeeleza kuwa linafuata maagizo ya kisiasa na liko tayari kwa hatua yoyote ya kuzuia meli hiyo kufika Gaza
Safari ya Handala
- Iliondoka Italia mnamo Julai 13, 2025
- Imebeba misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza
- Imefika umbali wa kilomita 194 kutoka Gaza mnamo Julai 26
- Imeanza kuelekea kusini karibu na pwani ya Misri baada ya kutambua meli za Israeli na droni zikikaribia