Wachezaji Wakosoa FIFA na Rais Gianni Infantino Kuhusu Kombe la Dunia la Klabu
Wachezaji wa soka wa kimataifa wameikosoa vikali FIFA na Rais wake Gianni Infantino kufuatia kuongezwa kwa Kombe la Dunia la Klabu hadi timu 32, likifanyika katika msimu wa mapumziko ya ligi za ndani
Muungano wa wachezaji wa kimataifa (FIFPRO) ulisema:
Soka linahitaji uongozi wa kuwajibika, si wa kifalme.” Walisema FIFA inafanya maamuzi bila kuwashirikisha wachezaji, ikiwemo kuongeza idadi ya mechi bila muda wa kupumzika kimwili na kiakili.
🌡️ Wachezaji walilalamika kuhusu hali ya hewa kali, wakicheza mechi mchana kwa joto kali ili kuvutia watazamaji wa kimataifa. Mashindano hayo yaliungwa mkono na fedha kutoka Saudi Arabia, yakileta faida kubwa kwa vilabu, lakini bila mashauriano rasmi na wachezaji.
FIFPRO iliongeza:
Ni jambo la kusikitisha kuona mashindano yakifanyika katika mazingira hatarishi kwa afya ya binadamu, hata kwa wanamichezo wa kiwango cha juu.
FIFA haijatoa tamko rasmi kuhusu malalamiko hayo, huku FIFPRO ikisisitiza kuwa haki za wachezaji zinadhoofishwa na mfumo wa utawala wa kiimla wa FIFA.
Toa Maoni