Hispania, Ireland na Ufaransa Kuitambua palestin
Katika hatua ya kihistoria inayoongeza kasi ya msukumo wa kimataifa wa kutambua uhuru wa Palestina, serikali za Hispania 🇪🇸 na Ireland 🇮🇪 zimekaribisha rasmi uamuzi wa Ufaransa 🇫🇷 kutambua Dola ya Palestina ifikapo mwezi Septemba 2025, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Uamuzi huo umetangazwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akisisitiza kuwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha suluhisho la mataifa mawili kati ya Israel na Palestina linadumishwa.Pedro Sánchez, Waziri Mkuu wa Hispania, alisifu hatua hiyo akisema: "Pamoja lazima tulinde suluhisho la mataifa mawili ambalo Netanyahu anajaribu kuliharibu."
Muhtasari wa tamko hilo:
- Canada na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 24 walisaini tamko la pamoja wakitaka vita Gaza kukoma mara moja.
- Tamko hilo linakemea vikali mauaji ya raia wa Palestina wanaotafuta msaada wa kibinadamu. Linaitaka Israel kuondoa vikwazo vyote vya usambazaji wa misaada na kuruhusu mashirika ya kibinadamu kufanya kazi kwa usalama.
- Linalaani pia mpango wa Israel wa kuhamisha kwa nguvu raia wa Gaza na kupanua makazi ya walowezi, jambo linaloathiri suluhisho la mataifa mawili.