picha-ya-watu-wa-gaza
iliandikwa Julai 25, 2025 picha-ndogo-ya-mwandishiNa Twaha Ahmadi 2,456

Mapokezi ya kihistoria kwa Georges Abdallah baada ya kifungo cha miaka 41

Katika tukio lililogubikwa na hisia na historia, maelfu ya wananchi wa Lebanon walimiminika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beirut leo kumpokea Georges Ibrahim Abdallah, Ambaye amerejea nyumbani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 41 nchini Ufaransa.

Abdallah, mwanaharakati wa zamani wa kikomunisti na mwanzilishi wa kundi la FARL, alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 1987 kwa kuhusika na mauaji ya wanadiplomasia wa Marekani na Israeli.

Licha ya adhabu hiyo, amekuwa ishara ya upinzani na mshikamano kwa wafuasi wa harakati za ukombozi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kauli Kali ya Abdallah Baada ya Kufika

Watoto wa Gaza ni mifupa inayotembea, huku mamilioni ya Waarabu wakitazama tu. Ni wakati wa kusimama na kupambana.” β€œIsrael inaishi sura za mwisho za uwepo wake

Abdallah alipokelewa kama shujaa – huku wafuasi wakipeperusha bendera za Lebanon, Palestina, na vyama vya mrengo wa kushoto. πŸ“ Amekwenda kijijini kwake Qobayat, ambako maandalizi ya sherehe za mapokezi yamepamba moto.

Toa Maoni